![]() |
Na Angela Sebastian-Bukoba
Naibu waziri wa maji Mhandisi Mathew Kundo ameagiza wakala wa maji Vijijini- RUWASA- mkoani Kagera kuwapatia kiasi cha milioni 100 mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira BUWASA ili wampatie mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wa Bugashani ili akamilishe mradi huo uliokwama.
Mhandisi Kundo ametoa agizo hilo wakati alipotembelea eneo palipojengwa matenki ya maji ya mradi huo utakaonufaisha wananchi wa kata tano,uliopo kata ya Buhembe na kuzungumza na wananchi na watumishi wa mamlaka zote za maji za mkoa wa Kagera.
Kundo amesema kuwa Serikali haipo tiyali kuona wananchi wake wakiteseka kwa kukosa huduma ya maji hivyo pesa hiyo inatakiwa kupatiwa mkandarasi haraka iwezekanavyo ili ifikapo Septemba mwaka huu mradi huo uwe umekamilika ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.
Kadhalika ameongeza kuwa Serikali haipo tayari kuwavumilia wakandarasi wazembe wanaokwamisha miradi ya maji na kupelekea wananchi kupata adha ya kushindwa kunufaika na miradi hiyo, kwa wakati badala yake wakandarasi hao wataondolewa kwenye mfumo wa kupewa miradi mipya ya maji.
Pai amepiga marufuku mamla zote nchini kuongeza ankara zisizoendana na matumizi sahii ya mteja.
Naye Naibu waziri mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato amesema, mradi huu utakaogarimu bil 3.3 ambapo kwa kiasi kikubwa fedha nyingi imeishaletwa ingawa mradi umechukua muda mrefu anatarajia kunufaisha kata tano za Manispa ya Bukoba.
Alisema gharama za kuunganisha maji ni kubwa hivyo amemuomba Rais wa Jamhur ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan aone ni namna gani watausaidia katika changamoto hiyo.



Comments
Post a Comment