Na Emmanuel Chibasa.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Alfred Mtambi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika semina ya maswala ya uwekezaji na vivutio vinavyotolewa na serikali kwa wawekezaji kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC),
Semina iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara inatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne 23 Julai,2024 katika ukumbi wa uwekezaji uliopo Musoma mkoani Mara.
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Mara una idadi ya watu 2,372,015 kutoka 1,743,830 wa sense ya mwaka 2012. Mkoa wa huu umebarikiwa fursa nyingi za uchumi na uwekezaji kupitia sekta mbalimbali kutokana na uwepo wa hifadhi ta Taifa ya Serengeti ambayo asilimia 70 inapatikana mkoa wa Mara, Ziwa Victoria ambalo ni Ziwa la tatu kwa ukubwa duniani na visiwa vinavyo patikana pia katika ziwa hili vinatoa fursa kubwa za kijamii, kiuchumi, uvuvi, Utalii na umwagiliziaji.
Jamii ya wakazi wa mkoa wa Mara wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mazao,ufugaji, uvuvi, utalii, uchimbaji wa madini pamoja na biashara ya mpakani.
Ujio wa semina ya maswala ya uwekezaji na vivutio vinavyotolewa na serikali kwa wawekezaji kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania ni fursa kwa watanzania kutumia kituo cha uwekezaji kuwekeza katika mkoa wa Mara kutokana na fursa za uwekazaji Kilimo, ufugaji,utalii, uchimbaji madini,uvuvi pamoja biashara ya mpakani kutokana na serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.
Paschal Maganga ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania akiwa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera katika kampeni ya kuhamsisha uwekezaji wa ndani alisema katika kipindi cha kuanzia January hadi June 2024 miradi 409 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.09 tayari imesajiliwa katika kituo hicho na kwamba inatarajiwa kutoa ajira 121,209 pindi itakapo kamilika.
Katika jitihada za kuhamasisha uwekezaji wa ndani Kituo cha uwekezaji, Tanzania inaendesha kampeni ya kuhasisha uwekezaji wa ndani kwa kutoa elimu kwenye mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkoa wa Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Ruvuma, Lindi, Rukwa, KIgoma na Katavi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) Kwa upande wa Unguja na Pemba.

Comments
Post a Comment