Mbunge Vedastus Mathayo Atembelea Hospitali ya Manispaa ya Musoma Aahidi Kutatua Changamoto ya Vifaa Tiba
Na Shomari Binda-Musoma
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe.Vedastus Mathayo ametembelea hospitali ya Manispaa ya Musoma na kukutana na Mganga mMfawidhi ili kujua changamoto za huduma.
Mhe.Mathayo ametembelea hospitali hiyo leo julai 17, 2024 na kulidhishwa na upatikanaji wa dawa licha ya changamoto ya upungufu wa baadhi ya vifaa tiba.
Akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo Dk.Emanuel Shani, amesema huduma bora za afya ni muhimu kwa wananchi na ndio kilichopelekea kuitembelea hospital hiyo.
Amesema amelidhishwa kusikia dawa zinapatikana na wananchi wanapofika wanahudumiwa na kupatiwa dawa kwa wsnaohitaji na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.
Mbunge huyo amesema changamoto alizoambiwa za upungufu wa vifaa tiba hasa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura anakwenda kufanyia kazi kwa kuwasiliana na Wizara ya afya.
" Kila ninapotoka bungeni napita kwenye maeneo yanayotoa huduma za jamii jimboni kujua changamoto na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi kabla sijaanza mikutano ya hadhara.
Nimeamua kuanzia sekta ya afya kwa kufika hospital ya manispaa ya Musoma na ninashukuru kusikia uhakika wa upatikanaji wa dawa na ndio wananchi wanachohitaji",amesema
Aidha mbunge mathayo ameishukuru serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya bilioni 1 kwaajili ya ukarabati wa hospital hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya magonjwa ya kinywa na meno pamoja na macho.
Awali akimpa taarifa Mhe mbunge, Mganga mfawidhi wa hospital ya manispaa ya Musoma Dk.Emanuel Shani amesema uhakika wa upatikanaji wa dawa hupo hospitalini hapo kwa kuwa wakiagiza wanazipata kwa wakati kutoka bohari ya dawa MSD kanda ya ziwa.
Amesema ili Hospital hiyo iendelee kupata dawa na vifaa tiba vya kutosha kwa wakati inapaswa kuwekwa kwenye orodha ya hospital mpya zilizoanzishwa.
Mbunge Mathayo ameanza ziara ya kuzunguka maeneo mbalimbali jimboni ili kuelewa na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi.




Comments
Post a Comment