Kizza Besigye afikishwa mahakamani Uganda

GEORGE MARATO TV
0




 Kizza Besigye amefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Makindye, nchini Uganda.


Wanachama wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC ) leo walipiga kambi katika Mahakama hiyo, wakisubiri kufikishwa kwake mahakamani, gazeti la Monitor limeripoti.

Kiongozi huyo mkongwe wa upinzani aliripotiwa kutoweka mwishoni mwa juma katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi alikokuwa ameenda kwa shughuli binafsi.

Siku ya Jumatano, vyanzo vilisema Dk Besigye, mmoja wa wanasiasa waliokamatwa mara nyingi zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Uganda, alirejeshwa nchini na alikuwa akishikiliwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye na alitakiwa kufikishwa mahakamani.

Kutoweka kwa Besigye kulifuatia kukamatwa Julai 23 kwa wanaharakati 36 wa Uganda wanaohusishwa naye huko Kisumu, mji wa kando ya ziwa nchini Kenya karibu na mpaka.

Wanaharakati hao wa kisiasa walitekwa nyara na kusafirishwa hadi Uganda ambako walifunguliwa mashtaka ya uhaini na kupelekwa katika Gereza la Kitalya.

Wanaharakati hao ambao waliachiliwa kwa dhamana hivi karibuni, walikana mashitaka hayo na kusema walikuwa wakihudhuria warsha walipokamatwa. Wanaharakati hao 36 wanadai kuteswa wakati wa kuzuiliwa kwao.

 Besigye ashtakiwa kwa makosa ya kukutwa na silaha

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda inamshtaki Besigye kwa makosa manne ikiwemo kupatikana na silaha katika hoteli moja jijini Nairobi na kujadiliana kuhusu silaha na wageni huko Geneva, Athens na Nairobi.


Yeye na mwenzake Obedi Lutale wamekanushwa mashtaka

Amerejeshwa rumande hadi Desemba 2.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top