TRA Yawashauri Wananchi Umuhimu wa Kudai Risiti Wanaponunua Bidhaa

GEORGE MARATO TV
0



 Na Angela Sebastian-Bukoba

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA ) imewashauri wananchi kutambua umuhimu wa faida za kudai na kutoa risiti pindi wanaponunua na kuuza bidhaa kwani hiyo inasaidia na kuwalinda pale ikatokea changamoto hususani wizi,pia  inaongeza ulipaji kodi kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa na Afisa uhusiano mkuu kutoka TRA makao makuu Hudson Kamoga wakati akiongea na waandishi wa habari wa  mkoa wa Kagera katika mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na mamlaka hiyo, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa elimu juu ya kazi zinazofanywa na TRA hususani wajibu wa ulipaji kodi kwa ihari.


"Wanaponunua na kudai risiti wanatimiza wajibu wako kisheria,ni uzalendo kwa nchi yao pia ni ulinzi wa bidhaa waliyoinunua mfano amenua simu bila risiti ikatokea kuna mtu mwingine aliibwa simu kama ya kwako huwezi kujitetea kwamba hiyo ni mali yako kwasababu, huna uthibitisho ambao ni risiti inayoonyesha uhalali wa umiliki wa mali hiyo"anasema Kamoga

Amesema waandishi wa habari wanao wajibu wa kuelimisha jamii juu ya faida zinazotokana na ulipaji kodi ambapo faida moja wapo ni kuchangia asilimia 70 ya mapato ya Serikali na asilimia inayobaki inachangiwa na wahisani mbalimbali hivyo, akawaomba waendelee kutumia kalamu zao kuchochea maendeleo ya nchi ikiweko kueleza faida zitokanazo na kodi zao. 

Pia Afisa mwandamizi wa kodi TRA makao makuu Joel Lema amesema mtu anaponunua bidhaa akadai risiti anasaidia Serikali kukusanya mapato kwa urahisi ambapo inasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani ujenzi wa shule,barabara,vituo vya Afya na miundombinu ya maji hivyo,akawashauri wananchi kuendelea kulipa kodi ili Serikali iendelee kutoa huduma stahiki.

Naye meneja msaidizi mkoa wa Kagera huduma kwa mlipa kodi wa TRA mkoa huo Estomih Mossi amesema waandishi wa habari ni kiungo kati ya mamlaka hiyo na wananchi hivyo, kupitia vyombo mbalimbali vya habari wanaweza kutoa elimu ya mlipa kodi na kuwafikia kwa urahisi na haraka wananchi.

Rwekaza Rwegoshora ni Afisa elimu na mahusiano TRA mkoa wa Kagera akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari aliwasihi wafanyabiashara kutunza Kumbukumbu kwani inasaidia kutolipa kodi kubwa ukilinganisha na mitaji yao,pia kuepuka kulipa faini,kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja wanapokwepa kodi.

TRA mkoa wa Kagera kwa mwaka 2023/2024 walikusanya kiasi cha shilingi Trilioni 28 huku mwaka 2024 /2025 wanalenga kukusanya tril 30.4.  


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top