Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt.Tulia Ackson, leo tarehe 21 Oktoba, 2024 amefanya ziara ya kukagua mradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Mh Tulia amekagua miradi hiyo inayotekelezwa na Serikali kuu kwa uboreshaji wa shule ya sekondari Iganzo iliyopo Jijini Mbeya ambapo ilitengewa kiasi cha shilingi Milioni 174 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo.
Aidha mbunge huyo wa jimbo la Mbeya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini ikiwemo katika jimbo hilo.
Dkt Tulia amesisitiza kuwa Wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kulinda miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule kwakuwa elimu sasa ni bure.





