Serikali kukamilisha ujenzi wa bweni katika chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi Misungwi

GEORGE MARATO TV
0


Chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi(CDTTI)Misungwi kinahitaji kiasi cha shilingi billioni 1.9 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 352

Mkuu wa chuo cha hicho CHARLES ACHUODHO amebainisha hayo wakati wa ziara ya waziri wa maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalum DKT.DOROTHY GWAJIMA.

Achuodho amesema kuwa bweni hilo liko kwenye hatua ya msingi ambapo ujenzi wake tayari umeigharimu kiasi  shilingi millioni mia tatu.

Mradi wa ujenzi wa bweni hilo unatarajia kugharimu  kasi cha shilingi billioni 2.2 na kukamilika kwake kutaondoa adha ya wanafunzi wa chuo hicho  hususani wa kike kuishi mtaani.

Waziri GWAJIMA amekagua maendeleo ya ujenzi wa bweni hilo na kusisitiza dhamira ya serikali ya kukamilisha ujenzi wake.



Katika hatua nyingne dkt gwajma amewataka maafisa maendeleo ya Jamii nchini kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Pia amewaasa maafisa Hao kuwa mstari wa mbele katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top