Wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni mmiliki wa mtumbwi huo Amon Lutabanzibwa,Nahodha wa Mtumbwi Robert kabota na Msimamizi wa Mtumbwi Salum Shaban wote wakazi wa Jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza,Naibu kamishna wa polisi Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo baada ya Mtumbwi uliopinduka na kuzama kubainika kutokuwa na usajili wa kubeba abiria kutoka shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC)
Ajali hiyo ilitokea septemba 25 mwaka huu majira ya saa kumi na moja za jioni katika mwalo wa bwiru wilayani ilemela wakati mtumbwi MV SEA FALCON wenye namba za usajili TMZ 012212 Ukisafirisha abiria na mizigo kutoka mwalo wa kirumba kwenda kisiwa cha Goziba kilichoko kwenye ziwa Victoria wilayani Muleba Mkoani Kagera.
Waathirika 29 wa ajali hiyo waliokolewa na wavuvi kwa kushirikiana na polisi wanamaji baada ya kukutwa wakielea kwenye maji huku wakiwa wameshikilia madumu ya mafuta na wengine wakijitahidi kuogelea kwa ajili ya kujiokoa.
Majeruhi walifikishwa nchi kavu na kupatiwa huduma ya kwanza kisha walipelekwa hospitali ya mkoa ya Sekou-toure kwa matibabu ambapo 14 walitibiwa na kuruhusiwa na 15 bado wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Kamanda Mutafungwa amewakumbusha watoa huduma wa vyombo vya majini kuzingatia sheria na taratibu za usalama zinazowataka kutoa huduma ya usafiri kwa kuzingatia masharti ya leseni zinazotolewa na TASAC.
Pia amewataka wananchi kuendelea kupanda mitumbwi iliyosajiliwa kubeba abiria kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa maisha Yao.








Comments
Post a Comment