![]() |
| Aeleza kiwanda kilivyotengeneza ajira zaidi ya Elfu 11 kwa Vijana na Jinsi Rais Samia alivyoidhinisha Bilioni 344 kujenga kiwanda hicho. |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete aliambatana bega kwa bega na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ziara yake mkoani Morogoro ambapo Jana Jumatano Agosti 07, 2024 alishiriki kwenye Uzinduzi wa Kiwanda kikubwa cha Mkulazi- Mbigiri cha kuzalisha sukari takribani Tani Elfu 50 kwa mpigo kilichopo Kata ya Mkulazi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Waziri Kikwete amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni utashi binafsi wa Rais Samia kuirudisha Morogoro ya viwanda na dhamira yake ya kuongeza ajira kwa vijana ambapo baada ya kuapishwa kuwa Rais mara moja aliridhia ujenzi wa kiwanda hicho kwa kuidhinisha takribani Bilioni 344 ya ujenzi wake.
"Kiwanda hiki ni kielelezo cha ushahidi wa dhati kwamba Wewe (Rais Samia) ni Rais wa dhati unaposema au kuahidi unatimiza. Baada ya kuapishwa kuwa Rais mwezi wa 3, miezi 4 baadae yani mwezi wa 7 ulitoa maagizo ya kuruhusu uanzaji ujenzi wa kiwanda hiki. Umeanzisha ujenzi wa kiwanda hiki kwa nia yako nzuri ya kupambana na ile gap ya upungufu wa sukari nchini mwetu"
"Mhe. Rais uliruhusu Bilioni 344 zitengwe kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda na kuruhusu Jeshi la Magereza litoe ardhi ya ujenzi. Kiwanda hiki kimeenda kutatua kero ya ajira kwa vijana na katika ajira zote zaidi ya asilimia 92 ya kiwanda hiki ni za vijana wa Kitanzania" Alisema Waziri Kikwete akizungumza mbele ya Rais Samia kwenye uzinduzi wa kiwanda hiki mbele ya umati wa wananchi.




.jpg)


Comments
Post a Comment