Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhwani Kikwete ameshiriki kikao cha madiwani wa Chama Cha Mapinduzi ili kuchagua diwani atakayegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze.
Mh Kikwete ambaye ni waziri ofisi ya waziri mkuu,anayeshughulikia kazi,Ajira na watu wenye Ulemavu,ameshiriki kikao hicho ambacho kimefanyika Julai 26-2024 na kumchagua Bw Ramadhan Mawazo Mkufya kuwa mgombea kupitia chama cha Mapinduzi.
Bw Mkufya anbaye ni diwani wa Kata ya Kibindu,amepata kura 18 kati ya 19 zilizopigwa.



Comments
Post a Comment