Na Robinson Wangaso - Musoma.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi amewaasa waandishi wa habari kuutangaza mkoa wa Mara ili kuwavutia wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa ili kuweza kuwekeza katika mkoa wa Mara.
Kanali Mtambi ameyasema hayo leo Julai 5, 2024 katika ukumbi wa MK hotel iliyopo Mwisenge ndani ya Manispaa ya Musoma wakati wa Mdahalo uliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoani Mara na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Mara.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mkoa wa Mara unzazo fursa nyingi na Raslimali nyingi hasa madini ambayo yanapatikana katika maeneo mengi.
Hata hivyo Kanali Mtambi amesema mkoa wa Mara unayo historia kubwa kwani ndiyo mkoa alipozaliwa Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
" Naomba waandishi wa habari kuandika habari zinazoonyesha fursa zilizopo mkoani Mara ili kuhamasisha uwekezaji utakaokuza uchumi na kuleta maendeo". Alisema Kanali Mtambi mkuu wa mkoa wa Mara.
Mkuu huyo wa mkoa amesema waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa katika kuwajulisha wananchi juu ya fursa zilizopo mkoani Mara.
Amewataka waandishi wa habari kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi ya wanyamapori Serengeti, Ziwa Victoria na makumbusho ya Mwalimu Nyerere kijijini Butiama.
"Wadau wote wa maendeleo mkoani Mara mkiwemo waandishi wa habari, lazima tuungane katika kuhamasisha wananchi kuacha vitendo vya ukatili wa kijijsia na kuacha tabia za kujichukulia hatua mkononi" alisema Mtambi RC Mara .
Amesisitiza kuwa ili kupata mafanikio endelevu wadau wote waungane kuhimiza uendelevu wa fursa Kwa maendeo endelevu.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Klabu ya habari mkoani Mara Mgini Jacob amesema Klabu hiyo inakusudia kuanzisha Tuzo Kwa ajili ya waandishi wa habari watakaondika habari za kuutangaza mkoa wa MARA Kwa shughuli za uwekezaji na maendeo.
Akitoa mada katika warsha hiyo Boniphace Ndengo kutoka kampuni ya uwekezaji ya HAIPPA amesema kampuni za Umma zimetamkwa katika sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Mwaka 2004 ambapo kampuni za Umma ni mali ya wanaachi siyo Serikali ambazo zinaanzishwa ili kuvutia mitaji mikubwa ambapo mtu mmoja hawezi kumudu uwekezaji huo.
Ndengo amesema mkoa wa Mara hauna budi kujielekeza katika uanzishwaji wa makampuni ya Umma ili kuweza kurahisisha kukuza uchumi wa mkoa.
Naye mkurugenzi wa kiwanda cha Nyihita Sunflower Oil Production amesema wakulima na wazalishaji wa Alzeti katika mkoa wa Mara wajikite katika uzalishaji kwani kiwanda chake bado kinakabiliwa na uhaba wa malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya kula.
Kauli mbiu ya Mdahalo huo ni Mara Bora Kwa uwekezaji na kuishi umeandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mara na umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi.
.jpg)
Comments
Post a Comment