Na Emmanuel Chibasa
Mitandao ya kijamii kama Whatsapp, Facebook na Instagram imerahisisha mawasiliano kwa watumiaji kupata na kusambaza habari na kuwepo kwenye makundi mbalimbali.
Katika matumizi ya mitandao ya kijamii watumiaji huwa wanaunganishwa katika makundi mbalimbali na wasimamizi wa makundi hayo.
Kwa mujibu wa Muongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za Mawasiliano uliotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano wa mwaka 2019, Mtumiaji anapokua msimamizi wa kundi katika mitandao ya kijamii anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo.
1.Hakikisha unapata idhini ya mtumiaji kabla ya kumuunganisha kwenye kundi katika mtandao wa kijamii na kwamba anafahamu madhumuni na masharti ya kuzingatiwa anapojiunga na kundi unaloliratibu.
2.Hakikisha kama msimamizi wa watu walioko kwenye kundi lako, wanaelewa na kuzingatia na kujihadhari kuweka maudhui yasiyofaa kwenye kundi kwa mfano matusi, uchochezi, uzushi, n.k
3. Hakikisha watu waliopo kwenye kundi wanaelewa kwamba wana uhuru wa kutoka kwenye kundi mara wanapotaka kufanya hivyo na pia wanaweza kutolewa kwenye kundi na msimamizi wa kundi wanapokiuka matakwa ya sheria.
4.Hakikisha kama msimamizi wa kundi la mtandao wa kijamii unaelewa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015. Unaelewa kuwa sheria hii utamsaidia msimamizi wa kundi katika mtandao wa kijamii kutumia na kuratibu kundi lake la mtandao w kijamii vizuri zaidi.
Hakikisha kuwa una ufahamu wa kutosha kuhusu watumiaji wote au umetambulishwa na washiriki wengine unaowaamini waliounganishwa kwenye kundi unalolisimamia.
Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(Tcra)

Comments
Post a Comment