Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho, (Mb) tarehe 8 April, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Dola ya Qatari Nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi , Fahad Rashid AL-Muraikhi, jijini Dodoma
Balozi Fahad Rashid AL-Muraikhi alimueleza Waziri wa Ulinzi na JKT utayari wa Dola ya Qatari kushirikiana na Tanzania na katika masuala mbalimbali yanayohusiana na Wizara ya Ulinzi na Nchi kwa ujumla . Balozi Fahad Rashid AL-Muraikhi alisema Tanzania na Dola ya Qatari zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu ambayo yamekuwa ni chachu ya maendeleo baina ya Nchi hizo mbili , mahusiano hayo yamekuwa yakiongozwa na viongozi wakuu wa Nchi ya Tanzania na Dola ya Qatari ambapo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi Nchini Qatari mwaka 2023 . Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan Nchini humo ni kielelezo Cha utayari wa Tanzania kushirikiana na Dola ya Qatari katika nyanja mbalimbali za kiuchumi , utamaduni, ulinzi na kijamii na kuendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo ya muda mrefu
Naye waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, amemshukuru Balozi Fahad Rashid AL-Muraikhi kwa kufika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa ajili ya kiendeleza uhusiano wa kindugu na muda mrefu baina ya Tanzania na Qatari , Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho alimhakikishia Balozi Fahad Rashid kuwa Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano uliopo wa Nchi hizo mbili
Aidha Waziri Rhimo Nyansaho amemwambia Balozi Fahad Rashid utayari wa Wizara ya Ulinzi na JKT kushirikiana na Nchi ya Qatari katika masuala ya ushirikiano wa kijeshi, Mafunzo na kubadilishana utalaamu na kukabiliana na changamoto za kiusalama za ugaidi na uhalifu wa mtandaoni.
Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa waliokuwa na Waziri wa Ulinzi na JKT katika mazungumzo hayo ni pamoja na Kaimu Kamishina wa Utafiti na Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Josephy Kapumbe, na Mkurugenzi wa Huduma ya Mipango wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali Gerald Omary.


.jpg)
