KATIKA kipindi ambacho bei ya gesi ya kupikia duniani imepanda kwa kasi ya hadi asilimia 43, kampuni ya Taifa Gas imekuja na habari njema kwa Watanzania—hakutakuwa na ongezeko la bei ya gesi ya majumbani (LPG).
Hatua hii imepokelewa kama faraja kubwa kwa maelfu ya familia na wafanyabiashara wadogo wanaotegemea gesi katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 3, 2026, Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius, amesema kuwa soko la kimataifa limekumbwa na mabadiliko makubwa ya bei, hali iliyosababisha kuongezeka kwa gharama za ununuzi na usambazaji.
Amesema licha ya changamoto hizo, kampuni imechukua uamuzi wa kipekee wa kubeba gharama hizo ili kulinda wateja wake.
“Tunayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wateja wetu kwa kubeba athari za ongezeko la gharama ya nishati ya kupikia,” amesema Deogratius.
Aidha, Amesema Usambazaji Waendelea Kuimarishwa Mbali na kudhibiti bei, Taifa Gas pia imehakikisha kuwa upatikanaji wa gesi hautatetereka.
"Kupitia mtandao wa maghala 25 nchini kote, kampuni inaendelea kusambaza gesi kwa uhakika mijini na vijijini". Amesema
“Tanzania ni nchi kubwa na yenye mahitaji tofauti… upatikanaji wa nishati hii ni kipaumbele kikubwa kwetu,” amesisitiza Deogratius.
Kadhalika amesema katika Hatua ya Kuelekea Nishati Safi kwa Wote Uamuzi huu unaonyesha dhamira ya Taifa Gas ya kuendelea Kupanua matumizi ya nishati safi Kutoa huduma nafuu,Kujenga mfumo imara wa usambazaji Katika wakati ambao gharama za maisha zinaendelea kupanda, hatua kama hizi zinaonyesha jinsi sekta binafsi inavyoweza kuwa sehemu ya suluhisho.
Wakati dunia ikikumbwa na kupanda kwa bei ya gesi, Taifa Gas imechagua njia tofauti ili kulinda wateja wake badala ya kuongeza mzigo kwao.


