Tofauti za Mishahara Kwa Watumishi wa Umma Kushughulikiwa-Waziri Mkuu

GEORGE MARATO TV
0


Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imebaini kuwepo kwa tofauti kubwa ya mishahara kati ya watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi, hali inayohitaji hatua za haraka ili kurekebisha uwiano huo.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma, Dkt. Nchemba amesema jumla ya watumishi wa umma 7,447 wanapokea mishahara isiyoendana na majukumu yao, ambapo hadi Machi 26 mwaka huu, walilipwa mishahara ya binafsi yenye gharama ya shilingi bilioni 14.34.



Amesema Serikali imeona umuhimu wa kuchukua hatua za kupunguza tofauti hiyo kwa kuwianisha viwango vya mishahara ili kuhakikisha malipo yanalingana na kazi zinazofanywa na kuondoa upungufu uliopo kwa baadhi ya watumishi.

Aidha, Serikali imepanga kuhuisha sheria ya utumishi wa umma pamoja na kanuni zake zinazohusu utoaji wa vibali vya mishahara binafsi, sambamba na kufanya mapitio ya waraka unaohusu utaratibu wa kushughulikia maombi hayo ili kuongeza uwazi na ufanisi.

Hatua hizo zinatarajiwa kuboresha mfumo wa malipo kwa watumishi wa umma na kuleta usawa zaidi katika sekta ya ajira nchini.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top