Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mheshimiwa Lukuvi Atakumbukwa Kwa Mengi -Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, Mheshimiwa William Lukuvi atakumbukwa kwa mengi na Watanzania kutokana na utumishi wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali alizohudumu.

“Mheshimiwa Lukuvi atakumbukwa kwa mengi na Watanzania kutokana na utumishi wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali. Mchango wake kwa Jamii na Watanzania kwa ujumla katika nafasi mbalimbali alizotumikia kuanzia Chama, Jimboni na Serikalini umekuwa chachu katika kuleta maendeleo kwa wananchi,” amesema Waziri Mkuu ambaye ameongoza mazishi hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Machi 31, 2026) wakati akizungumza katika ibada ya mazishi ya marehemu iliyofanyika nyumbani kwake kwenye kijiji cha Idodi, wilayani Iringa, mkoani Iringa.


"Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nitumie nafasi hii kuwahahikishia kwamba jinsi alivyokuwa pamoja nanyi wakati wa uhai wake, na yale yaliyokuwa ndoto yake, yataendelea kutimizwa.

"Ni vema tukizingatia na kuyaishia yale tuliyoelezwa na viongozi wa dini pamoja na kwenye wasifu wake. Alikuwa akisisitiza ushirikiano baina ya Bunge na Mawaziri, leo hii tuyaenzi yote aliyoyasimamia."

Na kwa wana-Isimani, ninawasihi tuendelee kumuenzi, tusianze mashindano, tulinde heshima ya Mzee wetu kwa kuwa na staha."


Amesema Mheshimiwa Lukuvi alikuwa anajali maisha ya wale anaowaongoza na ndiyo maana ameweza kudumu jimboni kwa miaka 31. "Sisi wanasiasa tunajua, siyo kazi rahisi kuongoza kwa muda wote huo, lakini yeye aliweza kwa sababu aliweka kipaumbele  chake kwenye maisha ya wale anaowaongoza."

Amesema Serikali itaendelea kumuenzi kwa kuendelea kutekeleza miradi aliyoiacha hasa wa barabara ya lami ambayo alikuwa anaifuatilia sana. "Miradi ya Pawaga na Isimani yote itakamilishwa. Niwahakikishie kuwa Serikali itaendelea kuitekeleza kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM lakini pia sehemu ya kumuenzi Mheshimiwa Lukuvi," amesema. 

Naye Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu alisema kifo cha Mhe. Lukuvi kimeacha majonzi kwa kila mmoja na kwa uzito wa msiba huo,  Bunge limewakilishwa na wabunge 160.

"Mheshimiwa Lukuvi alikuwa anaujua uwezo wake na kifo chake ni pigo ambalo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepata kwa kuukosa umahiri wake Bungeni.

Mapema, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana wa CCM wajifunze na waige mapito ya Mhe. Lukuvi ambaye alianzia ngazi za chini kabisa hadi akafika kwenye uongozi wa Taifa.

"Mwaka 1974 alijiunga na chama cha TANU, akajiendeleza hadi kufikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana."

Alisema jambo kubwa la kujifunza kutoka kwa Mhe. Lukuvi ni jinsi alivyoweza kulea jimbo ilhali ana majukumu makubwa ya kitaifa. "Siyo wengi ambao anakuwa Mbunge au Waziri halafu analea jimbo. Watu aina hii wako wachache sana. Wengi wakipata vyeo wanasahau majimbo na kuja kuwaona wapigakura wakati wa uchaguzi," alisema na kushangiliwa. 

Alisema kuweza kudumu kwenye madaraka na Marais wanne tangu awamu ya Rais Mkapa hadi sasa, ni ishara tosha kwamba aliaminiwa na kuna jambo la kujifunza kutoka kwake. "Marais wote hawa walikuwa na watu wao, lakini kwa kuendelea kuwa naye, ina maana alikuwa na sifa na uwezo."

Ibada ya mazishi iliongozwa na Naibu Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Padre Paul Msombe ambaye alisisitiza kuwa ni vema kwatu wakaishi huku wakijiandaa kwa maisha ya baadaye mbinguni.

Akimzungumzia marehemu Lukuvi, Padre Msombe alisema: “Licha ya vyeo vyake alikuwa na unyenyekevu na mwenye kushirikiana na waumini wenzake.

 Tukumbuke kwamba ipo siku tutalala usingizi kama ndugu yetu William alivyolala usingizi wa amani. Kitu cha msingi ni kujiweka mikononi mwa Mungu, tufe katika BWANA. Hili ni suala la kila mmoja kujitazama na kujihoji kwamba mimi Mungu akiniita sasa hivi, ninaweza kusema nina haki ya kuingia mbinguni.?” 

Mheshimiwa Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa.


Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...