Mhe.Ghati Chomete Aipongeza Nyansaho Foundation Kwa Kuunga Juhudi za Rais Samia Mkoani Mara

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete Jana tarehe 22 Machi, 2026 alishiriki Hafla ya ugawaji saruji 6,000 kutoka Nyansaho Foundation kwa Wabunge wa Mkoa wa Mara.

Mhe.Ghati Chomete alimpongeza M/Kiti wa Taasisi ya Nyansaho ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Simeon Nyansaho kwa uamuzi wake wa kuunga juhudi za Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya maendeleo Mkoani Mara.


Mhe.Ghati Chomete ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Mara alimuhakikishia M/Kiti wa Nyansaho Foundation kwamba Wabunge wa Mkoa wa Mara wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa anatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia malengo ya kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Mara kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Mara maendeleo endelevu.

 Mhe.Ghati Chomete (Mb),

 Viti Maalum Mkoa-Mara,

 Machi 23, 2026

 Dodoma-Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top