Mkemia Mkuu wa Serikali Atoa 'shavu' Kwa Vijana wa Kitanzania

GEORGE MARATO TV
0


 DODOMA

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa fursa kwa vijana wabunifu wa Kitanzania wanaoweza kubuni na kuunda mifumo wezeshi ya TEHAMA na Akili Unde ili kuiwezesha serikali katika kuboresha utendaji kazi.

Akieleza utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na Fursa za vijana zilizopatikana katika Siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkemia Mkuu wa Serikali, Fedelice Mafumiko amesema fursa hiyo kwa vijana wabunifu ni dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifanya nchi kuwa na wataalamu wengi katika sekta Mbalimbali hapa nchini.


"Wabunifu wa Kitanzania wanaoweza kubuni na kuunda mifumo wezeshi ya TEHAMA na Akili Unde watasaidia kupunguza gharama za uendeshaji na kupunguza urasimu katika utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau mbalimbali". Amesema 

Sambamba na hayo, Mkemia Mkuu huyo amesema Pamoja na Mamlaka kuendelea na utaratibu wa Kutumia wataalam wake wa ndani kufanya matenegenezo na matengenezo kinga ya mitambo na vifaa vya maabara lakini Bado hutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.

"Mamlaka inatarajia kukabiliana na changamoto hizi Kwa kuendelea kuwajengea uwezo wa kitaalam watumishi wa Mamlaka ili wawe mahiri na wabobevu katika eneo la matengenezo na matengenezo kinga ya mitambo na kupunguza utegemezi wa Wataalam kutoka nje ya nchi". Amesema 

"Mamlaka pia inatoa fursa kwa vijana wenye ujuzi wa kutengeneza Mitambo ya uchunguzi kuja Kutoa huduma hiyo". Amesisitiza




Katika hatua nyingine, amesema Mamlaka imepanga kuendelea kuimarisha huduma za maabara kwa kununua mitambo mikubwa ya kisasa pamoja na vifaa saidizi na vitendanishi kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.

Amesema pia Mamlaka inapanga kuimarisha miundombinu kwa kujenga ofisi na maabara katika ofisi za kanda ikiwemo Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini, kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

"Mamlaka itaendelea kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama pamoja na urasimu katika utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau mbalimbali". Amesisitiza

Katika kipindi Cha January 2025 Hadi Februari 2026 Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilifanikiwa kufanya uchunguzi wa kisayansi Kwa jumla ya vielelezo/ Sampuli 247,286 sampuli zilizochunguzwa na Mkemia Mkuu wa Serikali zilizotokana na kuongezeka Kwa uelewa wa wananchi na wadau wa mamlaka pamoja na ubora wa huduma za uchunguzi zitolewazo na Mamlaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top