Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Nassirya Nassir Ally amewataka wazazi na walezi kuwatunza watoto wote bila ubaguzi, hususan watoto wenye ulemavu, huku akisisitiza kuwa kuwaficha watoto hao kunawanyima haki zao za msingi na fursa za kuonesha vipaji na uwezo walionao katika jamii.
“Nitoe wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu, Watoto hawa wana uwezo mkubwa kama watoto wengine na wakipewa malezi bora, elimu na mazingira rafiki wanaweza kufanya mambo makubwa na kuisaidia jamii na Taifa letu.”
Kongamano hilo limewakutanisha wanawake kutoka makundi mbalimbali, viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala ya haki za wanawake, usawa wa kijinsia, ujasiriamali na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.





