WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 27, 2026 ameshiriki ibada ya kuaga mwili wa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongoza waombolezaji katika tukio hilo.








