Agnes Marwa Atoa Tuzo kwa Shule za Sekondari Zilizofanya Vizuri Manispaa ya Musoma

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, leo ametoa tuzo na zawadi maalum kwa shule za sekondari zilizofanya vizuri katika Manispaa ya Musoma, ikiwa ni hatua ya kutambua na kuhamasisha ubora wa elimu mkoani humo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika ndani ya Manispaa ya Musoma, Agnes Marwa amekabidhi tuzo kwa shule zilizopata matokeo bora katika Mtihani wa Kidato cha Nne, sambamba na kuwazawadia walimu wa masomo yaliyopata alama A pamoja na mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwa kupata Daraja la Kwanza (Division I.7) Thelesia Obotto anayetokea Shule ya Sekondari Bweri, jambo lililopokelewa kwa shangwe na pongezi kutoka kwa viongozi na wadau wa elimu waliohudhuria hafla hiyo.


Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, ambaye aliambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa Mh. Alex Nyabiti, Waheshimiwa Madiwani, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara  pamoja na Katibu wa UWT Mkoa na viongozi wengine wa chama na serikali.





Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Agnes Marwa amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo ni sehemu ya dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kuhamasisha ushindani chanya miongoni mwa walimu na wanafunzi.

“Walimu ni nguzo muhimu katika kujenga Taifa lenye wasomi na wataalamu. Tunapowatambua na kuwapongeza, tunawatia moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi,” alisema Agnes Marwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Juma Chikoka aliwataka walimu na wanafunzi kuendeleza ari ya kufanya vizuri zaidi, akisisitiza kuwa mafanikio ya elimu ni msingi wa maendeleo ya Mkoa wa Mara na Taifa kwa Ujumla na pia amempongeza Mh Agnes kwa kufanya Tukio kubwa Linaloacha alama ya faraja na motisha kwa walimu na wanafunzi wa Manispaa ya Musoma, huku likidhihirisha mshikamano kati ya viongozi, wadau wa elimu na jamii katika kuinua kiwango cha taaluma mkoani Mkoa wa Mara.


Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Ndg Idd Mkoa amempongeza Mh Agnes Marwa kwa kujitolea kwake na kuwataka wabunge wote wa Mkoa wa Mara kuiga mfano wa Mbunge Agnes Marwa.


















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top