📌 *Wananchi wapewa elimu ya nikonekt* .
📌 *Wananchi waaswa kutunza na kulinda ya umeme* .
📍 *PANGANI*
Wakala wa vijijini (REA) umeendelea na zoezi la uhamasishaji kujiunga na huduma ya umeme.
Uhamasi umefanyika wilayani Pangani umeme ambapo mamlaka ya REA na TANESCO wametembelea nyumba ambazo zimenufaika na miradi ya umeme pamoja na mikutano ya hadhara yenye lengo kuu la kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na huduma.
Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi amesema,
Kwa sasa taratibu za uombaji huduma ya umeme zimeboreshwa zaidi na hakuna tena mambo ya kutumia kufanya maombi ambapo kwa kutumia namba ya Nida mwananchi anaweza kufanya ombi la umeme moja kwa moja TANESCO kupitia huduma ya NIKONEKT.
“Kwa kutumia simu janja, mwananchi atapakua huduma ya Nikonekt na kufanya maombi au kama simu ya kawaida atabonyeza *152*00# na kisha kufuata maelekezo ya kufanya ombi, hakuna wakala wanaosajili maombi mtaani tafadhali tuepushe vishoka” mkomi alisisitiza.
Aidha mkomi ameongezea kuwa, pamoja na umeme kufika majumbani ni vyema wananchi walio na eneo la mradi wakachangamka na kutumia fursa hiyo kujiunga mapema na huduma ya umeme.
Aidha, wananchi wameombwa kuendelea kutunza umeme umeme kwani mpaka umeme unafikishwa katika na au kitongoji umesafiri kutoka mbali sana na umepita katika njia salama ndio maana unawaka, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza ya kulinda ili kulinda usalama wote.
Halikadhalika, uelimishaji huu utaendelea wilaya kwa wilaya, Kata kwa kata kijiji cha kijiji cha kitongoji mkoani Tanga.
Vilevile, REA itaendelea kutekeleza na miradi tofauti ya umeme ikiwa ni pamoja na kupeleka umeme kwenye vitongoji na miradi ya ujazili ili kuhakikisha kila mwananchi wa mkoa wa Tanga hususani mwananchi aishie kijijini na pembezoni jiji anafikiwa na huduma ya umeme.
Mwisho.





