Na. Mwandishi wetu, Zanzibar.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, katika kikao chake kilichofanyika Zanzibar tarehe 25 Januari 2026, imeidhinisha uteuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi mbalimbali wa chama wanaotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi.
Kwa upande wa Tanzania Bara, wajumbe walioteuliwa kuingia Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni Paul Christian Makonda na Livingstone Joseph Lusinde (wanaume), pamoja na Asia Abdulkarim Halamga (wanawake).
Kutoka Zanzibar, Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Khamis Mussa Omar (wanaume) na Tauhida Cassian Galos (wanawake).
Aidha, Kamati Kuu imemteua Agnes Elias Hokororo kuwa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, huku Najma Murtaza Giga, Deodatus Philippo Mwanyika na Cecilia Daniel Pareso wakiteuliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge.
Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Said Ali Juma na Hamza Hassan Juma (wanaume), pamoja na Lela Muhamed Mussa (wanawake).
Vilevile, Machano Othman Said ameteuliwa kuwa Katibu wa Wawakilishi wote wa CCM, huku Mahmoud Omar Hamad na Hudhaima Mbarak Tahir wakiteuliwa kuwa Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi.
Katika uamuzi mwingine muhimu, Kamati Kuu ya CCM, kwa mujibu wa Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la Julai 2025, imemteua Dkt. Lazaro Killian Komba kuwa mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Peramiho, wilayani Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Hatua hizi zinaonesha wazi mwelekeo wa CCM kuimarisha safu ya uongozi wa chama na kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi katika chaguzi zijazo.














Comments
Post a Comment