Siku 100 za Dkt. Samia Suluhu Hassan Serikali Imekutana na Wanaume Ili Kuondoa Tatizo la Ukatili wa Kijinsia Nchini
DODOMA.
Kutokana na umuhimu wa wanaume katika ustawi na maendeleo ya jamii, Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na majukwaa mbalimbali ya wanaume nchini ili kuona namna Bora ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuimarisha malezi, makuzi na wajibu wa familia katika jamii.
Kauli hiyo ya serikali ameisema waziri wa maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dorothy Gwajima Leo jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya utambuzi,urasimishaji na uwezeshaji wa makundi ya wajasiriamali katika sekta isiyo Rasmi ndani ya siku Mia Moja za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema hatua hiyo ya ushirikishwaji wa wanaume ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha majukwaa ya wanaume kwa lengo la kutambua mchango wao katika ustawi na maendeleo ya jamii.
"kwa kuelewa umuhimu wa wanaume katika ustawi na maendeleo ya jamii yetu, Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na majukwaa mbalimbali ya wanaume nchini ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha majukwaa ya wanaume ili waisaidie serikali Kwa sehemu kubwa". Amesema waziri Gwajima
Sambamba na hayo, Waziri Gwajima amesema ili kuimarisha malezi na makuzi ya watoto chini ya miaka 8 ambao ndio msingi imara wa rasilimaliwatu yenye tija siku za baadaye, serikali kupitia wadau wa maendeleo imekamilisha utengenezaji wa Mfumo wa kufatilia masuala ya malezi na makuzi ya Watoto katika jamii kupitia Kadi ya Upimaji (ECD - Score Card).
"Tumeandaa Dash Board kwa lengo la kukusanya takwimu na taarifa zinazotokana na mifumo ya Wizara na Taasisi kisekta zinazotekeleza afua za malezi na makuzi ya mtoto wadogo ili kubaini ulinganifu katika utekelezaji wa afua za afya, elimu ya awali, lishe na ulinzi pamoja na usalama wa mtoto". Amesma
"Sekta zote zinatakiwa kutekelezwa kwa uwiano ulio sawa". Amesisitiza
Aidha, Waziri Gwajima amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imepokea jumla ya Shilingi Billion 10.5 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ya asilimia saba kwa mwaka kwa wafanyabiashara ndogondogo.
"Tayari jumla ya Shilingi 1,351,660,000.00 zimetolewa kwa wafanyabiashara 588 kupitia mfumo wa Benki ya NMB na zoezi la utoaji mikopo linaendelea nchi nzima". Amesema.
Serikali imesema zoezi la urasimishaji kwa kundi la waendesha pikipiki maarufu bodaboda na bajaji linaendelea ambapo imewahimiza wengine waendelee kujitoke ili wapate mikopo inayotolewa na serikali.







Comments
Post a Comment