WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 23, 2026 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda, kukagua Meli ya Ambulance, kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Kusukuma na Kuhifadhi Maji, pamoja na kuzindua Meli ya MV Mwanza.
Meli hiyo ya MV Mwanza inatarajia kufanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba huku ikitarajia pia kufanya safari zake kati ya Mwanza na nchi jirani ya Uganda.
Taarifa ya serikali ilitolewa mwaka jana wakati meli hiyo ikitengezwa ilisema pia MV Mwanza itafanya safari nyingine kati ya Mwanza na Musoma baada ya kukamilika kwa kazi ya marekebisho ya bandari ya Musoma.







Comments
Post a Comment