Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (mb) , tarehe 21 januari 2026, jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe Balozi Andrew Lentz
Pamoja na masuala mengine viongozi hao wamejadili kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili . Aidha viongozi wawili Tanzania na Marekani walijadili masuala yahusuyo ulinzi na usalama pamoja na uchumi ambao nchi hizo zimekuwa zikishirikiana.
Dkt.Nyansaho ameishukuru serikali ya Marekani na Balozi Lentz kwa kufika na kumuona na serikali ya Marekani kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania wakati wote tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo ambao umekuwa na faida kwa maslahi mapana kwa wananchi wa pande zote mbili
Naye kaimu Balozi wa Marekani Nchini Mhe.Balozi Andrew Lentz ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano wake na serikali ya Marekani.









Comments
Post a Comment