Umoja wa Madiwani CCM umesikitishwa na kitendo cha kuchapishwa na kusambazwa kwa ujumbe unaohusu Posho za waheshimiwa Madiwani, Ujumbe uliochapishwa na kusambazwa kupitia Account ya Kigogo Kigogo katika Mtandao wa Facebook.
Aidha Umoja huo Umeutaarifu umma wa Tanzania kupuuza ujumbe huo wa upotoshaji na uchochezi unaolenga kuichafua serikali pamoja na Heshima ya Waheshimiwa Madiwani Nchini.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Karibu wa Madiwani wa CCM Tanzania Hilda kadunda pamoja na kulaani vikali tulip hilo imeviomba vyombo vya dola pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini kuwachukulia hatua wote wanaohusika ili kukomesha kabisa za Wanaharakati wachochezi na Wasiolitakia Mema Taifa.
"Madiwani wa Tanzania tunao utaratibu rasmi wa kuwasiliana na serikali yetu kwa Jambo lolote na kwa wakati wote, Hivyo Madiwani kwa umoja wetu Tunamshukuru kwa dhati Rais wetu Mpendwa Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa msikivu na Mwenye kujali maslahi ya Waheshimiwa Madiwani"imeeleza Sehemu ya Taarifa hiyo.




