Iran Yaonya: Kukosekana Kwa Makubaliano Kutaendeleza Vita

GEORGE MARATO TV
0


 Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limetangaza kuwa, licha ya shinikizo la muda mrefu kutoka kwa maadui wake kutaka kusitishwa kwa mapigano, Tehran ilisimama imara na kukataa hadi sasa ilipoona malengo yake ya kijeshi yanafikiwa.

Katika taarifa hiyo, Iran imesema kuwa baada ya takribani siku 40 za vita, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika operesheni zake na imewaweka maadui katika hali inayodai ni ya udhaifu mkubwa. Hata hivyo, imeonya kuwa mapambano yanaweza kuendelea ikiwa mafanikio hayo hayatatafsiriwa katika ushindi wa kisiasa na usalama wa kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa kufuata mwongozo wa viongozi wake wa juu, Iran sasa imekubali kuingia katika mazungumzo na Marekani, yatakayofanyika mjini Islamabad, nchini Pakistan kuanzia Ijumaa ijayo. Lengo la mazungumzo hayo Baraza limesema ni kuweka mfumo wa makubaliano ya kudumu ndani ya kipindi kisichozidi siku 15.

Iran imesisitiza kuwa imewasilisha mapendekezo yake yenye masharti maalumu 10 kupitia Pakistan, ambayo ndiyo mpatanishi mkuu. Kwa mujibu wa Tehran, upande wa Marekani umeonyesha utayari wa kuyatumia kama msingi wa majadiliano, licha ya vitisho vya awali vilivyotolewa hadharani.

Hata hivyo, Iran imeweka wazi kuwa mazungumzo hayo hayaashirii mwisho wa vita. Badala yake, ni sehemu ya mwendelezo wa mapambano kwa njia ya kisiasa. Imeongeza kuwa iwapo makubaliano hayatafikiwa, itaendelea na operesheni zake za kijeshi bila kusita.

Baraza hilo pia limewataka wananchi wa Iran kudumisha mshikamano wa kitaifa na kuunga mkono mchakato wa sasa wa mazungumzo, huku likionya kuwa nchi iko tayari kujibu kwa nguvu kubwa hatua yoyote ya uhasama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top