Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI tisa waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wiki ijayo wakikabiliwa na tuhuma za kudharau na kukaidi amri halali ya mahakama, hatua inayoweka hatarini kupelekwa kifungo kwa miezi kadhaa.
za uhakika zinasema kesi hiyo tayari imesajiliwa mahakamani kwa namba 000014659, ikidai kuwa viongozi hao waliendelea shughuli za kisiasa hadharani licha ya kuwepo taarifa ya muda wa mahakama iliyowazuia kufanya hivyo hadi pale wa kesi ya msingi utakapotolewa.
Imeelezwa kuwa tangu kutolewa kwa zuio la mahakama, viongozi hao hawapaswi kufanya shughuli za kwa mwamvuli wa chama au kutumia ofisi na mali nyingine za chama, imedaiwa kuwa wamendelea kufanya hivyo kinyume na amri ya mahakama.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, viongozi hao wanaweza kupandishwa kizimbani wakati wowote wiki ijayo kujibu mashtaka ya kudharau amri ya mahakama (contempt of court).
Viongozi wa CHADEMA waliotajwa katika kesi hiyo ni:
1.John Heche – Makamu wa CHADEMA Bara.
2.John Mnyika-Katibu Mkuu wa CHADEMA
3.Amani Golugwa – Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara
4 Godbless Lema – Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini
5.John Pambalu-Mmoja wa Wakurugenzi wa CHADEMA
6 Boniface Jacob – Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani.
7.Pamela Maassay – Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA)
8.Hamad Musa Yusufu – Kiongozi Mwandamizi wa CHADEMA
9.Gervas Lyenda-Kada mwandamizi wa CHADEMA.
Walalamikaji na Vyeo vyao vya Zamani
Walalamikaji katika kesi hiyo ni wanachama wa zamani wa CHADEMA waliowahi kushika nyadhifa muhimu ndani ya chama:
Said Issa Mohammed – aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar,Ahmed Rashid Khamisi pamoja na Maulidah Anna Komu.
Walalamikaji wanadai kuwa viongozi hao walifanya mkutano wa kisiasa, kutoa matamko na shughuli za chama hadharani, hatua inayohusishwa na ukiukwaji wa amri ya mahakama iliyowataka kusubiri kesi ya msingi.
Chanzo cha Kesi
Kesi hiyo inatokana na shauri la msingi huru lililofunguliwa na walalamikaji wakipinga baadhi ya maamuzi na shughuli za viongozi wa chama hususani ukosefu wa usawa kwenye Mgawanyo wa fedha za ruzuku baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kufuatia shauri hilo, mahakama ilitoa amri ya muda (temporary injunction) ikiwazuia viongozi hao kuendelea na shughuli za kisiasa kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Hata hivyo, walalamikaji wanadai kuwa viongozi hao waliendelea na shughuli za kisiasa kinyume na zuio la mahakama, jambo lililosababisha kufunguliwa kwa shauri jipya la kudharau amri ya mahakama.
Hatari ya Adhabu
Wataalamu wa sheria wanasema kuwa mahakama itathibitisha ukiukaji huo, viongozi hao wanaweza kukabiliwa na Faini, au Kifungo cha miezi sita sita.
Kesi hiyo hutawala nchini hisia kubwa za kisiasa na kisheria, huku wadau wakisubiri hatua za mahakama zitachukuliwa katika siku zijazo.







