Mbunge wa Jimbo la Kyerwa Akoshwa na Utendaji wa Waziri Ulega

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian; Kyerwa

Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, mkoani Kagera Khalid Nsekela, amemshukuru Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega kwa kuchukua hatua madhubuti na kufika jimboni humo kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Omurushaka–Karagwe hadi Rwenkorongo (Kyerwa) ambapo amesema ni uthibitisho kwamba Serikali ya hawamu ya sita inajali wananchi wake.

Hatua hiyo ya Ulega imetokana na mbunge huyo baada ya kuuliza swali bungeni wiki hii kuhusu ujenzi wa barabara hiyo usivyolidhisha na kusababisha wananchi kupata adha wakati wa kusafiri hususani wagonjwa na wajawazito ambapo waziri huyo alitoa majibu na kuahidi kufika kujionea hari hiyo ndani saa 72 ambapo ametekeleza ahadi hiyo.

Nsekela amesema barabara hiyo imekuwa kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Kyerwa kutokana na umuhimu wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa zao.

“Barabara hii ilikuwa imekwama kwa muda mrefu na imekuwa kilio kikubwa cha wananchi wa Jimbo la Kyerwa. Niliwasilisha ombi hili bungeni nikitambua mateso ambayo wananchi wangu wamekuwa wakiyapitia, hivyo napenda kumpongeza Waziri wa Ujenzi kwa kusikiliza na kuchukua hatua madhubuti niseme Rais Dk .Samia Suluhu Hassan hakukosea kukuweka katika nafasi hii" amesema Nsekela.

Alisema utekelezaji na ufuatiliaji wa karibu wa mradi huo unaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya hawamu ya sita katika kutatua changamoto za wananchi, hususan waishio maeneo ya vijijini,maana hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali ya hawamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu inajali wananchi wake pia ni sikivu.

Aidha Nsekela aliwapongeza wananchi wa Kyerwa kwa kuendelea kumuunga mkono na kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo Imani ya wananchi hao kwake na Serikali ya CCM ndiyo inampa nguvu ya kuendelea kupigania miradi ya maendeleo.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top