Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya siku 100, Wizara ya Madini kupitia Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) ipo katika hatua za mwishoni za usimikaji wa mtambo wa kusafisha chumvi katika eneo la Llingaula Wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Hayo yamebainishwa Leo January 26,2027Jijini Dodoma na Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati akieleza ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika kipindi Cha siku 100 alizowaahidi Watanzania kipindi Cha uchaguzi Mkuu.
Amesema hatua hizo za mwishoni za usimikaji wa mtambo wa kusafisha chumvi ni mojawapo ya uongezaji thamani madini ya chumvi.
"Gharama za ujenzi zinakadiriwa kuwa Shilingi Bilioni 4 na uwezo wake utakuwa ni wastani wa tani 2,040 kwa mwezi ambapo ni sawa na tani 24,480 kwa mwaka". Amesema
"Wavunaji wa Chunvi kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara watanufaika na huduma zitakazotolewa na Mtambo huo unatarajiwa kuanza kazi Februari, 2026". Ameongeza
Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza hatua za awali za ujenzi wa Maabara kubwa na ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini katika eneo la Kizota mkoani Dodoma, yenye ukubwa wa mita za mraba 8,258 hatua inayolenga kuimarisha sekta ya madini na kuongeza thamani ya rasilimali hiyo hapa nchini.
"Maabara hiyo inaukubwa wa Mita 8,258.3 na ujenzi wake unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 14.3". Amesema
Sambamba na hayo, Waziri Mavunde Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 Wizara imesimamia masoko 44 na vituo vya ununuzi wa madini 114 na kuwezesha biashara ya madini yenye thamani ya jumla ya Shilingi trilioni 4.031 kufanyika katika masoko hayo.
"Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2025 biashara ya madini yenye jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 3.102 ilifanyika katika masoko na vituo vya madini nchini". Amesema
"Hadi sasa kuna jumla ya masoko 44 na vituo vya ununuzi 117 nchini". Ameongeza
Kwa Upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi Mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan umeimarisha Sekta ya Madini hapa nchini.
Wizara inaendelea na ukamilishaji wa Mkakati wa Uongezaji Thamani Madini wa miaka mitano (5) kuanzia 2026/2027 hadi 2030/2031 ambapo Kupitia mkakati huo, ujenzi wa viwanda vya uongezaji thamani utafanyika katika Mikoa sita ya Kimadini ambayo ni Arusha, Dodoma, Kahama, Mbeya, Lindi na Pwani.





Comments
Post a Comment