WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza maalumu la Bunge la mashabiki wa Simba na Yanga Jumamosi Januari 31, 2026 ambapo Banking ya Azania ndio wazamini wakuu katika Bonanza hilo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, Festo Sanga, ametoa kauli hiyo leo wakati akitambulisha bonanza hilo katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo pia amekabidhi vifaa kutoka Benki ya Azania huku akiipongeza Bank hiyo Kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha.
Amesema Bank ya Azania imekuwa ikionesha ushirikiano mkubwa Kwa Serikali Kwa miaka minne mfululizo.
"Kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu tunaishukuru sana Azania Bank Kwa kuendelea Kutoa ushirikiano wao katika sekta ya Michezo". Amesema
Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Azania, Elizabeth Nyattega amesema benki yao itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusaidia sekta ya michezo.
"Azania Bunge Bonanza tumewza kudhamini Bonanza hili vizuri mnoo, na tunaamini Michezo inaunganisha jamii, pia Bank ya Azania itaendelea Kushirikiana na Serikali". Amesema.
Bunge Azania bonanza litafanyika viwanja vya Shule ya John Merlin, Miyuji jijini Dodoma na litashirikisha watumishi wa bunge, wabunge na pia timu kutoka wizara mbalimbali na mashabiki wa Simba na Yanga wa Dodoma ambapo zaidi ya michezo 21 itakuwepo, ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, kikapu, wavu, riadha, mbio za gunia na mingineyo.











Comments
Post a Comment