Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Mhe. Fadhili Maganya, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mhe. Christopher Gachuma, Mtoto wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wazee zaidi ya 160, wazee wameazimia kulinda na kudumisha amani na utulivu katika Mkoa wa Mara na kufanya kikao kama hicho kila mwaka.















