Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene ameweka wazi umakini na uthubutu wa aliyekua Mbunge na Waziri aliyehudumu wizara mbalimbali,Marehemu Jenista Mhagama wakati wa Bunge lililokuwa na Upinzani mkali akiwataja baadhi ya waliopata kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Godbless Lema,Freeman Mbowe na Dkt Wilbrod Slaa.
Ameyasema hayo leo alipofika kutoa pole kwa wafiwa katika eneo la Itega jijini Dodoma ambapo viongozi mbalimbali pia walifika kutoa pole kwa familia na wafiwa.





