Na Angela Sebastian ;Bukoba
Makamu wa Rais Mh Dk.Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam tawi la Bukoba kinachojengwa kata Kalabagaine kijiji Itahwa halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa ameyaswma hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema uzinduzi huo utafanyika Desemba 15 mwaka huu ambapo pia uzinduzi huo utaudhuliwa na Rais mstaafu wa hawamu ya nne Dk.Jakaya Mlisho Kikwete ambaye ni mkuu wa chuo hicho huku akieleza kuwa uwepo wa chuo hicho unakwenda kufungua fursa katika mkoa huo.
Naibu mratibu wa mradi wa chuo hicho Profesa Liberato Haule amesema chuo hicho endapo kitakamilika ,kitakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 800 na awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 chuo kitapokea wanafunzi 660 awamu ya kwanza ambapo huku matarajio yao ifikapo 2030 wafikie wanafunzi 1600 na kusema kuwa chuo hicho kitatoa masomo ya biasha na tehama pia kutakuwa na kituo cha kutoa ushauri kwa wafanyabiashara.



