Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi

GEORGE MARATO TV
0

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria kwa kutumia usafiri wa magari mawili tofauti ya abilia.

Taarifa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, Novemba 23, 2025 wilaya ya Sengerema wakati akizungumza na umma kupitia vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mafanikio ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao yametokana na  ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu na uwekaji wa vizuizi barabarani: Katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, jumla ya wahamiaji haramu 13 walikamatwa tarehe 23.11.2025 majira ya 7.30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata yenye usajiri T. 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari zake kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.

Wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alifanikiwa kutoroka eneo la tukio na jitihada za kumsaka zinaendelea.

Watuhumiwa wengine waliohusika katika usafirishaji walikamatwa ambao ni Mustahper Emily, miaka 24, Fundi magari, mkazi wa Kahama, Shinyanga na 

Pendo Matembere, miaka 36, Kondakta, mkazi wa Nyegezi, Mwanza.

Baada ya kuhojiwa, ilibainika kuwa wahamiaji hao waliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga, mkoani Kagera, mnamo tarehe 22 Novemba 2025.

Mtuhumiwa wa 14, Shadia Japhari Majaliwa, miaka 18, raia wa Burundi na mkazi wa Kisuru, aliokamatwa katika eneo la Nyatukara wilayani Sengerema akiwa ndani ya gari aina ya Yutong lenye namba za usajili T 131 DRE.

Magari yote mawili yamekamatwa na dereva pamoja na wasaidizi wengine wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Majina ya waliokamatwa ni:-

 1. Nkurunzinza Eloi, miaka 38, Mhuhutu, mkazi wa Muyinga, Burundi.

2.Bizimana Aster, miaka 20, Mhuhutu, mkazi wa Muyebe, Burundi.

3.Tanishaga Renova, miaka 20, Mhuhutu, mkazi wa Muyebe, Burundi.

4.Nyosaba Anatory, miaka 23, Mhuhutu, mkazi wa Muyebe, Burundi.

5.Niyokuru Jlock, miaka 23, Mhuhutu, mkazi wa Muyebe, Burundi.

6.Nsolimana Evariste, miaka 30, Mhuhutu, mkazi wa Ngozi, Burundi.

7.Riyazimana Jerome, miaka 30, Mhuhutu, mkazi wa Ngozi, Burundi.

8.Mbonipa Claude, miaka 23, Mhuhutu, mkazi wa Ngozi, Burundi.

9.Ntirampera Oleste, miaka 42, Mhuhutu, mkazi wa Nyanzalaki, Burundi.

10.Mbalishimana Swalidi, miaka 47, Mhuhutu, mkazi wa Kitega, Burundi.

11.Sindobizero Osca, miaka 28, Mhuhutu, mkazi wa Tangala, Burundi.

12.Irakize Derise, miaka 27, Mhuhutu, mkazi wa Ngozi, Burundi.

13.Elias  Sinilemeya, miaka 31, Mhuhutu, mkazi wa Kitega, Burundi.

14.Shadia Jafari, miaka 18, Mrundi, mkazi wa Kisuru, Burundi.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha doria na vizuizi vya barabarani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na wananchi ili kudhibiti matukio ya kihalifu. Aidha, amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwafichua wahalifu popote walipo, ili waweze kudhibitiwa kabla hawajafanya uhalifu wowote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top