Watanzania Waombwa Kuliombea Taifa Kuelekea Uchaguzi Mkuu

GEORGE MARATO TV
0


 Taasisi ya TANZANIA JUMUISHI imetoa wito kwa watanzania juu ya kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani huku ikihimiza watanzania kufanya ibada ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika mwezi oktoba 29.

Akisoma Tamko hilo mapema hii leo, oktoba 25, 2025, Innocent Gabriel Siriwa, Katibu wa Taasisi ya TANZANIA JUMUISHI (TAJU), Yenye lengo kuu la kuzitambua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini, ambapo amesema kwa nia nzuri na ya kizalendo imeona iitishe hafla hii ili kuhamasisha kuombea amani uchaguzi mkuu.

Aidha, Innocent amesema kuwa jamii imekuwa ikisahau juu ya uwepo wa watu wenye ulemavu hivyo uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchqguzi mkui ni wazi kuwa jamii inashindwa kujali uwepo wa idadi kubwa itakayoathirika ya kundi la watu walemavu.

Hata hivyo, Taasisi hiyo ya TAJU kupitia Katibu wake ndugu Innocent Gabriel Siriwa imewaomba viongozi na wasimamizi wa uchaguzi wa mkuu wa mwezi oktoba kusimamia kwa weledi na haki ili kuendelea kuhimarisha hali ya amani iliyopo nchini.

Kwa upande wake, Emmanuel Majeshi ambaye ni Mratibu wa Dawati la utetezi la watu wenye ulemavu- THRDC, amesema kuwa amani inapotoweka katika jamii kundi linalo athirika moja kwa moja ni watu wenye ulemavu hivyo ametoa wito kwa watanzania kuilinda amani iloyopo kuelekea uchaguzi mkuu wa oktoba 29.

Sambamba na hilo Majeshi amesema kuwa zipo jitihqda mbalimbali zinaendelea kufanywa na viongozi wa dini juu ya umuhimu wa haki na amani hivyo watanzania wanatakiwq kuwa sehemu ya kudumisha amani kwa maslai ya taifa.

Serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali nchini wamekuwa nguzo muhimu katika kutoa elimu na hamasa juu ya umuhimu wa utunzaji wa amani nchini Kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo utunzaji wa amani ni jambo la kila mmoja wetu kwani kuna maisha baada ya uchaguzi wa oktoba 29, 2025.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top