Eng Magesa Mwita Aipongeza Shule ya Sekondari ya Morembe-Musoma Mjini

GEORGE MARATO TV
0

 


Mhandisi Mwandamizi katika Sekta ya Ujenzi, Eng. Magesa Mwita amesema hatua ambayo inachukuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa shule za mchepua wa Sayansi na ufundi nchi nzima itawezesha kutoa jawabu la tatizo kubwa la ajira kwa vijana nchini.

Mhandisi Magesa ametoa kauli hiyo Oktoba 16 mwaka huu 2025 mjini Musoma  wakati akihutubia wanafunzi,walimu na wazazi wa shule ya Sekondari ya Morembe katika mahafali ya kidato cha nne ya wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa shule hizo kwa kila mkoa nchini  kama moja ya mkakati wa kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kukabiliana na tatizo la ukisefu wa ajira kwa vijana 

Kwa sababu hiyo amewapongeza wahitimu katika mahafali hayo, huku akitoa wito kwa wanafunzi wote kuweka mkazo kwa masomo ya mchupua wa Sayansi kwani amesema kufanya hivyo kutawawezesha kufika mbali na kumudu changamoto za kimaisha.

"Wanafunzi wote wekeni mkazo kwenye masomo ya Sayansi, na yale yenye kuwapa ujuzi mbalimbali kama vile  ufundi,kilimo,ufugaji na ujasiriamali,tukifanya hivyo tutakuwa tunapata jawabu la tatizo la ajira kwa vijana"alisema mhandisi Magesa.

Aidha pamoja na kuwataka wanafunzi wa shule hiyo kuzingatia nidhamu,lakini pia amewapongoza kwa juhudi kubwa za kujisomea hatua ambayo  imeongeza ufaulu shuleni hapo.

"Hapa nawapongeza sana walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya hatua ambayo imeongeza ufaulu katika shule hii,lakini pia niwaombe endeleeni kufundisha kwa bidii na kuwajengea misingi vijana wetu katika kudumisha nidhamu"alisema

Kwa sabanu hiyo mhadisi Magesa ameipongeza serikali  kwa jinsi inavyoendelea na ujenzi wa madarasa,mabweni na maabara katika shule hiyo hatua ambayo imewapunguzia mzigo mkubwa wazazi katika kuchangia ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu

Katika mahafali hayo mhandisi Magesa ametoa TV smart  nchi 43 na King'amuzi cha Azam kwa ajili ya shule hiyo.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top