Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Ubunge Jimbo la Uyole kupitia CCM , Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Oktoba, 2025 ameshiriki katika ibada maalum ya kumuombea hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere katika siku ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere.
Ibada hiyo imefanyika Mkoani Mbeya katika kanisa la Hija Parokia ya Mwanjelwa ambapo mgeni rasmi katika Ibada hiyo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na kuongozwa na Askofu mkuu Gervas Nyaisonga wa jimbo kuu la Mbeya.







