Maelfu ya wananchi wa Nyamagana mkoani Mwanza wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Nyamagana wakiwa na hali ya shangwe lenye kuonesha wazi furaha yao katika kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ambaye tayari ameshawasili kwenye viwanja hivyo kwaajili ya kuanza kazi kubwa ya kunadi ilani ya uchaguzi ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake katika kuelekea miaka 5 ijayo.
Wananchi wa Mwanza wana jambo lao leo, endelea kufuatilia mbashara kujionea mwanzo mwisho kuepuka kupitwa na jambo hilo muhimu sanaa












