Rais Samia na Mkuu wa Majeshi Wamewezesha Ushindi Wangu-Simbu

GEORGE MARATO TV
0


 Mwanariadha Alphonce Simbu amewasili usiku wa kuamkia septemba 23 mwaka huu 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, akitokea Tokyo Japan kwenye mashindano ya Dunia ya mbio za Marathon kwa wanaume ambapo Simbu aliibuka mshindi na kupata medali ya dhahabu.

Akizungumza baada ya kupokelewa katika uwanja huo huo wa kimataifa Jijini Dar es salaam,Mwanariadha Alphonce Simbu amesema kuwa amefurahi sana kwa mapokezi makubwa aliyofanyiwa na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuweza kuweka mifumo wezeshi ya kurahishisha kupatikana vibali kwa wakati jambo ambalo husaidia kufikia malengo kiurahisi.

Aidha, Simbu amesema kuwa amekuwa akiutafuta ushindi huwo kwa zaidi ya miaka Kumi na amewataka wanamichezo wakitanzania kutokata tamaa katika kupambania ndoto za vipaji vyao kwani kufanya hivyo kutasaidia kufikia malengo waliyojiwekea.

Akizungumza kiongozi wa mapokezi hayo Kwa upande wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Jeshini, Luteni Kanali Penina Igwe,amesema jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania linampongezana Alphonce Simbu kwa ushindi huo wa kihistoria Uliochagizwa na uwepo wa mazingira wezeshi jeshini.

Aidha, Luteni Kanali amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana ni kutokana na mashirikiano ya shirikisho la riadha Tanzania na Wizara ya Michezo kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) jambo ambalo mashirikiano hayo husaidia kuibua vipaji mbalimbali kwaajili la Taifa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, amesema kuwa Simbu amejituma na amefanikiwa sababu ya uwepo wa mazingira wezeshi katika jeshi sambamba na uwekezaji wa Rais samia Suluhu Hasaan Katika jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Afisa Mteule daraja la pili na Kocha Mkuu wa Timu Teule ya Riadha ya jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Antony Muingereza amesema kuwa simbu ametutoa kimasomaso watanzania kwasababu ameandaliwa kwa kina. 

Nae, Mke wa Mwanariadha Alphonce Simbu, Rehema Daudi amesema kuwa anamshukuru mungu kwa ushindi huwo na kusisitiza kuwa Mungu amefanya mambo makubwa ya kushangaza katika mashindano hayo .








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top