▪️Bukoba, Kagera.
_Mkuu wa Mkoa atoa Mabati kuezeka Kanisa hilo, zaidi ya milioni 17 zapatikana kati ya 34 zinazohitajika._
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa kwenye Ibada na harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT, Mtaa wa Mishenye, Kata ya Butelankuzi lililopo Jimbo la Magharibi Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.
Mwaliko wa kushiriki Harambee hiyo ulitolewa na Askofu Msaidizi Prof. Josephat Rweyemamu.
Kwenye harambee hiyo, kiasi cha milioni 17,587,000 zilipatikana kati ya hitaji la milioni 31,100,000 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa alichangia mabati ya kuezeka Kanisa hilo pindi likikamilika.
Viongozi mbalimbali wa ushirika huo, Afisa Tarafa hiyo ya Rubale Ndugu Erick Ishengoma, Watendaji wa Kata na Vijiji mbalimbali walikuwepo pia.




