Muwasa Yapanda Miti Elfu Tano Kuhifadhi Mazingira

GEORGE MARATO TV
0


MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira (MUWASA) imefanikiwa kupanda zaidi ya miti 5000 kwenye eneo la Mradi wa chanzo cha maji uliopo mtaa wa Bukanga Kata ya Makoko Manispaa ya Musoma.

Lengo likiwa ni kutunza na kudumisha rasilimali za vyanzo vya maji hayo na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla katika eneo la mradi huo uliogharimu takribani shilingi Bilioni 56.7 ambapo chanzo kina ukubwa wa ekari 35.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Nicas Mugisha alisema kuwa eneo hilo linatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa uhuru Agosti 18, 2025 ambapo mradi huo utazinduliwa rasmi siku hiyo.

" Kinachofanyika hapa tumepanda miti rafiki wa vyanzo vya maji ili kutunza chanzo hiki cha maji na tumeazimia kupanda miti 6000 ndani ya ekari 14. 2 mradi huu ulianza mwaka 2019 ambapo tulipanda miti 300 na ikakua miti 263 na tumepanga kuhitimisha zoezi ifikapo Julai 2026" alisema Nicas.

Aidha  Mkurugenzi huyo wa Muwasa ametoa wito kwa wananchi kuacha kuharibu vyanzo vya maji kwa kutokufanya shughuli za kibinadamu eneo la mradi huo kama uchafuzi wa mazingira wa chanzo hiko cha maji kwa kuingiza ni mifugo eneo hilo la mradi wa wa upandaji miti.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo uliopo eneo la mradi Raphael Magiri alisema tunapoelekea kuupokea Mwenge wa uhuru mkoani hapa Agosti 15, 2025 tumewaelekeza wananchi kutokufua , kutokuosha  kuuingiza mifugo kwenye maeneo ya ziwa Victoria ambapo ndio chanzo icho cha maji.

" Kabla ya uwepo wa mradi huu kwa ujumla changamoto zilikuwa ni nyingi sababu wanawake walipata kazi sana ya kufuata maji mbali ziwa Victoria kwa ajili ya kuhudumia familia zao pia , baadhi ya wananchi walikuwa wakichafua mazingira ikiwemo kujisaidia ndani ya maji na kusababisha uwepo wa magonjwa ya homa ya matumbo na kichocho kwa sasa hali ni Tofauti na zamani, tunawaelekeza kuhifadhi mazingira hayo na wana tii" alisema Magiri.

Janet Patrick ni Mkazi wa mtaa huo pia ameshukuru serikali kwa kuuleta mradi huo ambao umewaondolea adha ya usumbufu wa kuamka alfajiri kwa ajili ya kufuata maji kwa kuwa maji hayo kwa sasa wanayapata kwa ukaribu sana baada ya kuunganishiwa mabomba katika makazi yao. 






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top