Rais wa Zamani wa Nigeria Jenerali Mstaafu Muhammadu Buhari amefariki dunia Nchini Uingereza alikokuwa kwa Matibabu.
Kufuatia kifo cha Buhari,Rais wa Nigeria Bola Tinubu amemwelekeza Makamu wake Kashim Shettima kwenda Nchini Uingereza kwa ajili ya kurejesha mwili wa Marehemu Nchini humo.
Rais Tinubu ametangaza kifo cha Mtangulizi wake Muhammadu Buhari siku ya Jumapili.
Buhari amefariki London siku ya Jumapili majira ya saa 5:30 za Jioni baada ya kuugua kwa Muda mrefu.
Tinubu tayari amezungumza na Mjane wa Marehemu Aishat Buhari na kuwasilisha Salamu zake za pole.
Marehemu Buhari aliongoza Nigeria kwa Mihula miwili Kati ya Mwaka 2015 na 2023.
Wakati wa uhai wake Jenerali Muhammadu Buhari pia amepata kuliongoza Taifa la Nigeria akiwa kiongozi wa Kijeshi Kati ya January 1984 hadi August 1985.
Rais Tinubu ameamuru Bendera kupepea nusu mlingoti ikiwa ni heshima kwa Hayati Muhammadu Buhari.