Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Julai 02 mwaka 2025 amezindua rasmi Mashindano ya Mkuu wa Majeshi (CDF CUP), huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha uzalendo, amani, mshikamano ukakamavu ikiwa na lengo la kuunga mkono dhamira ya amiri jeshi mkuu na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK SAMIA SULUH HASSAN katika kukuza sekta ya michezo hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, katika uwanja wa AZAM COMPLEX Dkt. Tax amesema kwakua michezo ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na taifa kwa ujumla, ni dhahiri kuwa upo muhimu kwa jeshi na wananchi kushirikiana katika kuinua na kuiendeleza sekta hiyo kikamilifu ambayo pia licha michezo kuwa sehemu ya mazoezi lakini pia inalenga kupata wanamichezo watakashindana kupata timu za jeshi kwaajili ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Aidha DK TAX amempongeza mkuu wa majeshi nchini Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuendeleza mashindano ya majeshi kwani licha ya kusaidia kuleta burudani lakini pia inasaidia kuongeza ukakamavu na utimamu wa mwili hususani katika suala la ulinzi wa amani.
Pia mh. wazir stergomena tax hakusita kuzungumzia uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika Oct. mwaka huu huku akiwataka wana michezo hao kushiriki uchaguzi huo ikiwa ni haki yao ya msingi kwa kuhakikisha wanashiriki kwa amani na utulivu.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Haji Othman, ameeleza faida za mashindano hayo ambayo ni mkakati wa Jeshi hilo katika kuimarisha afya na ustawi wa wanajeshi ikiwemo kuongeza mshikamano, nidhamu ufanisi ikiwemo kuongeza mahusiano kati ya jeshi na jamii.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo, Brigedia Jenerali Saidi Hamisi Saidi, ameitaja michezo iliyoongezwa mwaka huu kiwemo Mpira wa Miguu, wanaume.
Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa Netiboli, wanawake.
Mpira wa wavu, kwa wanaume na wanawake ,Mpira wa mikono, kwa wanaume na wanawake
Mpira wa kikapu, Wanaume na Wanawake
Mchezo wa Riadha, Wanaume na Wanawake.
Mchezo wa Ngumi, Wanaume na Wanawake.
Mchezo wa kulenga Shabaha, Wanaume na Wanawake ambapo michezo mipya iliyoongezeka idadi mitano ambayo ni Mchezo wa Kuogelea, Wanaume na Wanawake, Mchezo wa Kuruka vikwazo, Wanaume na Wanawake ,Mchezo wa Gofu, Wanaume na Wanawake na Mchezo wa Mieleka kwa Wanaume na Wanawake, Mchezo wa Vishale (Darts), kwa wanaume na Wanawake.
Aidha, kulingana na ongezeko la michezo vitatumika viwanja katika maeneo tofauti ikiwemo uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na klabu ya Azam, utatumika kwa ajili ya mechi za mpira wa miguu.
Viwanja vya Kambi ya Jenerali Twalipo – Mgulani, viwanja hivi vitatumika kwa ajili ya michezo ya Mpira wa kikapu, netiboli, mikono na wavu, vile vile michezo ya ngumi, kuruka vikwazo na mieleka ambayo nayo itafanyika Twalipo.
Viwanja vya Gofu Lugalo, utachezwa mchezo wa Gofu.Viwanja cha Msasani beach, mchezo wa vishale (darts).
Kiwanja cha 501 KJ (Lugalo), kitatumika kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu.
Makao Makuu ya Kamandi ya Wanamaji (Navy,) mchezo wa kuogelea utachezwa.


Comments
Post a Comment