Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Zamaless Development Foundation (ZDF) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini* amegawa jumla ya vitabu 14094, Kompyuta 9 na Printa 1 kwa Shule mpya na zenye ufaulu hafifu Msingi na Sekondari.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo *Mhe. Sagini* amesema kuwa vitakwenda kuchochea ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi kitaaluma na kupunguza adha kwa walimu ambao walikuwa wanaenda kuandaa mitihani nje ya shule jambo lilokuwa linasababisha uvujaji wa mitihani na ucheleweshaji.
Kwa upande wake *Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya Butiama Mwl. Baraka Alfred* amesema kuwa vitabu na vifaa vilivyotolewa na *Mbunge Sagini* vitasimamiwa kuhakikisha vinafanya kazi kama ilivyoelekezwa kwa walimu wakuu wa kila shule iliyopokea ili kufanikisha dhamira ya kuongeza ufaulu kwenye shule ambazo ufaulu wake upo chini na zile shule changa.
Naye *Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Zamaless Development Foundation (ZDF) Bw. Mbise Shauri* amesema kuwa moja kati ya malengo ya shirika hilo ni kuhakikisha wanakuza sekta ya elimu nchini hasa kwa wananchi waishio vijijini ambapo amewaomba wadau wa maendeleo kuwapa ushirikiano ili kufanikisha uimara wa shirika hilo na kulipeleka katika malengo endelevu ya 2025-2025.
"Shule za Msingi zilizofikiwa na msaada huu ni *Mganza, Bumangi, Singu Nyamikoma B, Nyamikoma A, Kyasamiti, Nyamisisi na Shule za Sekondari ni Masaba, Mirwa, Buhemba, Mmazami, Kemoramba, Wegero, Kirumi na Sagini* hivyo sina budi kumshuru *Mwenyekiti wa Shirika la (ZDF) Mhe. Sagini* kwa nguvu kubwa anayoitoa na *Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kutuandalia sera na miongozo mizuri mpaka kufanikisha zoezi hili," amesema Mbise.
Pia *Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Sagini Mwl. Anamaria Samson* amempongeza *Mbunge Sagini* kwa majitoleo yake ya mara kwa mara katika sekta ya elimu kwani amekuwa mfano bora katika juhudi za kuongeza ufaulu mashuleni na jitihada zake zinaonekana.
Aidha baadhi ya wanafunzi wamefurahishwa na msaada huo, *Yusuph Zakaria ni Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kyasamiti* amesema vitabu hivyo vitawasaidia katika kujisomea kwakuwa vimewekwa maarifa kwa upana zaidi.* Rejina Elijah ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Manyawa* amesema kuwa kompyuta hizo zitawapa wanafunzi motisha ya kusoma zaidi kutokana na ulimwengu wa sasa wa Teknolojia.












Comments
Post a Comment