Dc Chikoka Apokea Maaada wa Mabati Kutoka Nyansaho Foundation

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

TAASISI ya maendeleo ya Nyansaho Foundation imetoa msaada wa mabati 130 ya rangi yenye kiasi cha zaidi shilingi milioni 7 ili kusaidia kuezeka shule ya sekondari Rukuba.

Msaada huo umekuja kutoka taasisi hiyo kupitia wito wa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kuomba wadau mbalimbali kushiriki maendeleo ya elimu kwenye jimbo hilo.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuamua kusaidia.

Amesema zipo taasisi nyingi lakini Nyansaho Foundation imekuwa mfano wa kuigwa katika kusaidia na kutoa misaada kwa jamii ikiwemo ya kielimu.

Chikoka amesema shule hiyo itakapokamilika kwa asilimia mia moja itasaidia wanafunzi kupata elimu na kutovuka maji kwenda kupata elimu nchi kavu.

Mkuu huyo wa Wilaya amemshukuru mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt.Rhimo Nyansaho kwa msaada huo ambao kupitia wanafunzi kusoma inakuwa ni baraka kwa mkurugenzi huyo.

" Hili ni jambo la baraka lililofanywa na taasisi hii ambayo kwa mkoa wa Mara imekuwa msaada mkubwa kwa misaada wanayoitoa.

" Mabati haya tuliyosaidiwa yatakwenda kutusaidia kukamilishwa kwa shule na watoto wetu kupata sehemu sahihi pa kusomea",amesema.

Akizungumza na GMTV mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameishukuru taasisi hiyo kwa mchango waliotoa katika elimu ndani ya jimbo hilo.

Kwa upande wao wananchi wa Kisiwa cha Rukuba wameomba kufikishiwa salamu mkurugenzi wa taasisi hiyo kwwa kumshukuru kwa msaada alioutoa.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top