Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MRPC Yaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari



 Na Ada Ouko, Tarime.

CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Mara(MRPC), Kimefanya Maadhimisho ya siku wa Uhuru wa vyombo vya habari mei 23 mwaka 2025, Kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu kwa lengo la maendeleo ya tasnia ya habari.

Akifungua maadhimisho hayo, mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele alitoa wito kwa waandishi hao kuwa wazalendo, kwa kutathmini kazi zao, huku akiweka mkazo juu ya uweledi na ufanisi wa kalamu wanazotumia kuwa zinaweza kujenga au kubomoa jamii.

"Tunataka maendeleo makubwa ya vyombo vya habari, kwa hiyo tuitumie hii siku kujitafakari fanyeni tathmini ya kazi zenu kwa mwaka uliopita ili kubaini mapungufu na changamoto ili kwamba muweze kuongeza ufanisi wa kazi zenu" alisema Gowele

Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Mugini, amesema kuwa kauli mbiu hiyo kwa lugha ya kingereza "The impact of artificial intelligence on press freedom and media"kwa maana ya Mchango wa akili Mnemba kwa Uhuru wa vyombo vya habari, wakiwemo waandishi wa habari wenyewe inavyoweza kusaidia katika kuleta maendeleo kwa wanahabari na kwa jamii .

Uongozi wa chama hicho, ulifanikiwa kuteuwa baadhi ya wanachama wa MRPC walioshiriki na kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu kauli mbiu hiyo na kutoa elimu ya Akili Mnemba kwa Waandishi wa habari walioshiriki Maadhimisho hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa DimaOneline, Dina Maningo ni miongoni mwa waandishi wa habari walioshiriki semina za mafunzo ya (artificial intelligence ) kwa maana akili mnemba alitoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya akili mnemba kwa waandishi hao wa habari.

" Kupitia akili mnemba, unaweza kubaini taarifa halisi na taarifa feki, Kuna kitu kinaitwa google lens kwenye simu janja na kimpyuta kutumia app iyo unaweza kubaini picha na eneo ya picha husika mahali ilipo,anaeleza frat ladder twenty for pia inaweza kuonesha taarifa za usafiri wa anga kama ikiwa hauna mawasiliano ya msemaji wa serikali" alisema.

Amesema kuwa akili mnemba inaweza pia kupotosha na kwa kupunguza ubunifu wa kibinadamu kwa mtumiaji husika jambo ambalo anasema pia akili mnemba inaweza kutengeneza nyaraka bandia huku akisisitiza umakini zaidi mwandishi wa habari au muhariri atakae tumi akili mnemba kwenye kazi zake kwani ina uwezo pia wa kutengeneza taarifa zamani na kuwa taarifa za kisasa.

Fresha Kinasa, pia ni mmoja wa waandishi wa habari walioteuliwa na MRPC kutoa elimu ya akili mnemba kupitia mada ya 'Usalama Mtandaoni' (Digital Security) alieleza kuwa usalama mtandaoni ni hali ya mwandishi wa habari, vifaa vyake vya kazi na ujumbe anaoutoa kwa jamii vyote kwa pamoja vinakuwa katika hali ya usalama.

" Mwandishi wa habari katika kazi zako taarifa unazotoa kwa umma hakikisha ziko salama kwa maana ya wewe binafsi, vifaa vyako vya kazi kama kamera, simu na kompyuta vinakuwa salama endapo kompyuta yako haina usalama ni rahisi mtu kuiba taarifa zako" Anasema Kinasa.

Amesema ili mwandishi wa habari na vifaa vyake vya kazi kuwa salama kwanza anapaswa kutopenda kuchangia nywila (password) na mtu mwingine hata kwa mtua anayemfahamu, pia kuacha tabia ya kujihusisha na (Wi-Fi), kwakufanya hayo taarifa,habari huweza kudukuliwa.

Mwandishi wa Jambo Tv Helena Magabe, alieleza mafunzo aliyoshiriki yalikuwa yanahusu uandishi wa habari za uchuguzi, kwa kuzingatia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu utakaohusisha madiwani, wabunge na Rais.

Helena aliwaeleza wanachama na wasiowanachama wa MRPC katika kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba,2025, Mwandishi wa habari haruhusiwi kuajiriwa na mgombea kwa kufanya hivyo atapaswa kuacha kazi ya uandishi wa habari.

"Tumetakiwa kupitia tena sheria zilizotungwa mwaka 2024 na kanuni za mwaka 2025 zilizotungwa mwaka 1977, Sambamba na hilo kipindi cha uchaguzi tunapaswa kujali usalama wetu kwa maana ukihisi upotevu wa amani eneo la tukio chukua tahadhari kwa kuondoka haraka eneo hilo" Anasema Helena.

Maadhimisho hufanyika Mei 3 duniani Kitaifa yalifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita Mkoani Arusha ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, huku kauli mbiu ikiwa ni" The impact of artificial intelligence on press freedom and media' (Mchango wa akili mnemba kwa uhuru wa vyombo vya habari, Matumizi ya teknolojia hiyo kwa waandishi wa habari katiaka kuleta Maendeleo ya ukuaji wa sekta ya habari) 





























Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...