Na Shomari Binda-GMTV
KADA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dr.Wilson Maregesi Mukama amepongezwa kwa kuguswa na kusaidia jamii ya mkoa wa Mara maeneo mbalimbali.
Mukama amekuwa akisaidia jamii kwenye masuala ya afya,elimu,maji,michezo na masuala mengine kwenye jamii.
Hivi karibuni kwenye sekta ya michezo alipokuwa mgeni rasmi akifunga michezo ya Umitashumta mkoa wa Mara wilayani Tarime Dr.Mukama alichangia kiasi cha shilingi milioni 4 kwa timu ya mkoa kwaajili ya zawadi na maandalizi ya timu ya mkoa.
Akizungumza na GMTV kuhusiana na namna anavyoguswa na kuchangia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda kupitia ( UV-CCM) CDE.Fadhili Maneno amesema Chama cha Mapinduzi kinayo hazina ya kutosha ya watu wanaojitoa na kusaidia jamii.
Amesema Dr.Mukama amekua akisaidia jamii mara kwa mara kwenye maeneo mbalimbali na amekuwa mfano wa kuigwa.
CDE.Fadhili amesema suala la kutoa na kuchangia kwenye jamii sio kila mtu anaweza kufanya hivyo lakini kwa Dr.Mukama amekuwa akifanya hivyo mara zote.
Amesema kuchangia sekta ya michezo kwa timu ya Umitashumta mkoa wa Mara itasaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye mashindano ya kitaifa.
" Kwa moyo wa dhati nimpongeze kaka yangu Dr.Mukama kwa namna anavyoguswa na kujitoa kuchangia jamii yake.
" Tumemuona Tarime akichangia sekta ya michezo lakini sio kwenye michezo pekee amekuwa akionekana kuchangia shughuli nyingine za kijamii",amesema.
Hamis Magesa kutoka Kisorya Wilaya ya Bunda amesema wamekuwa wakiona Dr.Mukama akichangia maeneo mbalimbali na kuomba wadau wengine wenye nafasi na kuweza kutoa wachangie masuala ya jamii.
Hivi karibuni Dr.Wilson Mukama alichangia magodoro 30 kwa jamii iliyofikwa na majanga ya maafa ya mvua yaliyotokea mjini Musoma.




Comments
Post a Comment