JWTZ na Jeshi la India kushirikiana na mataifa tisa ya Afrika kukabiliana na matishio bahari ya hindi
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh dkt Stergomena Lawrence Tax amezindua zoezi la Pamoja la ulinzi wa Bahari maarufu kama ‘AIKEYME’ lenye lengo la kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu baharini katika ukanda wa Bahari ya hindi.
Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo aprili 13 mwaka 2025 katika bandari ya Dar es saam, baada ya kupokea meli vita moja kutoka nchini India ambayo imekuja maalum kwa ajili ya zoezi hilo linalohusisha nchi nyingine tisa za afrika, Mh, Stergomena Tax,amesema kuwa kumekuwa na matishio mbalimbali ya kiusalama baharini kama vile usafirishaji haramu wa madawa za kulevya,ugaidi,usafirishaji haramu wa bianadamu na uvuvi haramu.
Kwa sababu hiyo amesema kwa kushirikiana kwa Pamoja katika mazoezi hayo kutasaidia kuleta tija katika kushughulikia maswala hayo Pamoja na kuongeza ushirikiano na ujuzi katika ya nchi na nchi.
Waziri huyo wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,amesema kuwa uwepo wa mazoezi hayo ni moja ya matokeo ya jitihada za Mh. Rais Samia Suluhu Hassani katika kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali ikiwamo Pamoja na ziara mbalimbali za kitaifa anazozifanya katika kuimarisha ushirikiano na ya mataifa mengine.
Amesema kuwa nchi zote shiriki ikiwemo Tanzania zitakuja na vifaa na askari watakaoshiriki katika mazoezi hayo ikiwamo meli kubwa ya kisasa kutoka India itakayotumika katika mazoezi hayo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali Jacob John Mkunda amesema zoezi la AIKEYME litahusisha nchi hizo rafiki za afrika ikiwemo India na Tanzania hivyo inapaswa kuweka nguvu ya pamoja kukabiliana na matishio ya baharini.
Amesema tayari Tanzania imefanya mazoezi kama hayo na nchi za China na Marekani na hivi sasa linafanyika na nchi ya India ambapo nchi tisa rafiki zitashiriiishwa lengo likiwa kuweka nguvu ya pamoja ya kukabiliana na matishio hayo maeneo ya bahari.
"Hili ni zoezi la pamoja kati ya Tanzania na India,ni zoezi la kawaida kwani tulishafanya hivyo na wenzetu wa China na Marekani na sasa tunafanya na India lakini tutashirikisha mataifa tisa rafiki kwa lengo la kuweka nguvu ya pamoja ya kupambana na matishio baharini"alisema mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda.
Nae Waziri wa Ulinzi wa India, Mhe Rajnath Singh amewataka washirki kujiimarisha na kujidhatiti katika kufanya ulinzi kwenye ukanda wa bahari ya hindi kwani,amesema uwepo wa Bahari ya hindi ni chanzo cha Uchumi na ni uti wa mgongo katika mataifa mbalimbali mh rajnath singh-waziri wa ulinzi india.














Comments
Post a Comment